Mhubiri 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 2 (Swahili) Ecclesiastes 2 (English)

Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili. Mhubiri 2:1

I said in my heart, "Come now, I will test you with mirth: therefore enjoy pleasure;" and, behold, this also was vanity.

Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini? Mhubiri 2:2

I said of laughter, "It is foolishness;" and of mirth, "What does it accomplish?"

Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao. Mhubiri 2:3

I searched in my heart how to cheer my flesh with wine, my heart yet guiding me with wisdom, and how to lay hold of folly, until I might see what it was good for the sons of men that they should do under heaven all the days of their lives.

Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu; Mhubiri 2:4

I made myself great works. I built myself houses. I planted myself vineyards.

nikajifanyizia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna; Mhubiri 2:5

I made myself gardens and parks, and I planted trees in them of all kinds of fruit.

nikajifanyizia birika za maji, ya kuunyweshea mwitu mlimopandwa miti michanga. Mhubiri 2:6

I made myself pools of water, to water from it the forest where trees were reared.

Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng'ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; Mhubiri 2:7

I bought men-servants and maid-servants, and had servants born in my house. I also had great possessions of herds and flocks, above all who were before me in Jerusalem;

tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana. Mhubiri 2:8

I also gathered silver and gold for myself, and the treasure of kings and of the provinces. I got myself men-singers and women-singers, and the delights of the sons of men--musical instruments, and that of all sorts.

Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo. Mhubiri 2:9

So I was great, and increased more than all who were before me in Jerusalem. My wisdom also remained with me.

Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote. Mhubiri 2:10

Whatever my eyes desired, I didn't keep from them. I didn't withhold my heart from any joy, for my heart rejoiced because of all my labor, and this was my portion from all my labor.

Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua. Mhubiri 2:11

Then I looked at all the works that my hands had worked, and at the labor that I had labored to do; and, behold, all was vanity and a chasing after wind, and there was no profit under the sun.

Nikageuka ili kuipambanua hekima, na wazimu na upumbavu. Kwa maana mtu amfuataye mfalme afanye nini? Lilo hilo tu lililokwisha kufanywa. Mhubiri 2:12

I turned myself to consider wisdom, madness, and folly: for what can the king's successor do? Just that which has been done long ago.

Ndipo nilipoona ya kuwa kweli hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza; Mhubiri 2:13

Then I saw that wisdom excels folly, as far as light excels darkness.

macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa. Mhubiri 2:14

The wise man's eyes are in his head, and the fool walks in darkness--and yet I perceived that one event happens to them all.

Nikasema moyoni mwangu, Kama limpatavyo mpumbavu, ndivyo litakavyonipata mimi nami; basi, kwa nini nikawa na hekima zaidi? Nikasema moyoni mwangu ya kuwa hayo nayo ni ubatili. Mhubiri 2:15

Then said I in my heart, "As it happens to the fool, so will it happen even to me; and why was I then more wise?" Then said I in my heart that this also is vanity.

Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu! Mhubiri 2:16

For of the wise man, even as of the fool, there is no memory for ever, seeing that in the days to come all will have been long forgotten. Indeed, the wise man must die just like the fool!

Basi, nikauchukia uhai; kwa sababu kazi inayotendeka chini ya jua ilikuwa mbaya kwangu; yaani, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo. Mhubiri 2:17

So I hated life, because the work that is worked under the sun was grievous to me; for all is vanity and a chasing after wind.

Nami nikaichukia kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua; maana sina budi kumwachia yeye atakayenifuata. Mhubiri 2:18

I hated all my labor in which I labored under the sun, seeing that I must leave it to the man who comes after me.

Naye ni nani ajuaye kama huyo atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Hata hivyo atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo, ambamo ndani yake mimi nimeonyesha hekima chini ya jua. Hayo nayo ni ubatili. Mhubiri 2:19

Who knows whether he will be a wise man or a fool? Yet he will have rule over all of my labor in which I have labored, and in which I have shown myself wise under the sun. This also is vanity.

Kwa hiyo nikageuka kukata tamaa moyoni mwangu juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua. Mhubiri 2:20

Therefore I began to cause my heart to despair concerning all the labor in which I had labored under the sun.

Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili, nayo ni baa kuu. Mhubiri 2:21

For there is a man whose labor is with wisdom, with knowledge, and with skillfulness; yet he shall leave it for his portion to a man who has not labored for it. This also is vanity and a great evil.

Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua? Mhubiri 2:22

For what has a man of all his labor, and of the striving of his heart, in which he labors under the sun?

Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili. Mhubiri 2:23

For all his days are sorrows, and his travail is grief; yes, even in the night his heart takes no rest. This also is vanity.

Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu. Mhubiri 2:24

There is nothing better for a man than that he should eat and drink, and make his soul enjoy good in his labor. This also I saw, that it is from the hand of God.

Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi? Mhubiri 2:25

For who can eat, or who can have enjoyment, more than I?

Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo. Mhubiri 2:26

For to the man who pleases him, God gives wisdom, knowledge, and joy; but to the sinner he gives travail, to gather and to heap up, that he may give to him who pleases God. This also is vanity and a chasing after wind.